Mazingira FM

Majaliwa: Serikali itaimarisha miradi yote ya kimkakati

2 March 2024, 6:14 pm

Waziri mkuu Kasim Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kuimarisha miradi yote ya kimkakati na kupokea changamoto zote kupitia wabunge.

Na Adelinus Banenwa

Waziri mkuu Kasim Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kuimarisha miradi yote ya kimkakati na kupokea changamoto zote kupitia wabunge ambao ni mwakilishi wa wananchi .

Waziri mkuu amayasema hayo katika mkutano na wananchi Utegi wilayani Rorya ambapo amesema serikali kupia wizara ya Maji imeahidi kutoa Sh. Milioni 720 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji unaotoa huduma kata ya Komuge wilaya ya Rorya kwa ajili ya ujenzi wa tenki na chujio ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama.

Majaliwa amesema serikali kuna maeneo mengi ambayo wanayagusa kama wizara ya Afya, maji, kilimo ,elimu umeme, miongone mwa maeneo mengine, Pia amesema kukamilika kwa ujenzi wa chuo cha veta wilayani Rorya utakapo kamilika kitapokea wanafunzi wote kwa ajili ya kuwapatia vijana ujuzi utakao wawezesha kujitengeneza ajira.

Hata hivyo majaliwa amesisitiza namna ambavyo watumishi wanavyopaswa kuwahudumia wananchi huku akiwataka watumishi kutenga siku kwa ajili ya kuwatembelea wananchi kuwasikiliza na kutatua changamoto na kero zao waziri mkuu ametembelea wilaya ya Rorya na kukagua mradi wa maji komuge, kukagua hospital ya wilaya ya Rorya, na kuhitimisha kwa kufanya mkutano na wananchi katika uwanja wa osongo .