Mazingira FM

Mwili mwingine wa mchimbaji wa madini wapatikana mgodi wa Kinyambwiga

31 December 2023, 7:09 pm

Mwili mwingine wa mchimbaji wa dhahabu mgodi wa dhahabu wa  Kinyambwiga  wilayani Bunda umeopolewa zikiwa ni siku 21 tangu taarifa za kufukiwa na kifusi Dec 09, 2023.

Na Adelinus Banenwa

Mwili mwingine wa mchimbaji wa dhahabu mgodi wa dhahabu wa  Kinyambwiga  wilayani Bunda umeopolewa zikiwa ni siku 21 tangu taarifa za kufukiwa na kifusi Dec 09, 2023.

Akizungumza na Mazingira fm kamanda wa polisi kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa mara Mrakibu wa polisi AGOSTINO MAGERE amesema mwili wa mchimbaji huyo aliyetambulika kwa jina la Joseph Matias  Joseph mkazi wa Katoro Geita umeopolewa jana Dec 29, 2023 na umekabidhiwa  kwa ndugu ili kuendelea na utaratibu mwingine.

Aidha kamanda Magere ametoa wito kwa wachimbaji wote mkoa wa Mara kuchukua tahadhari hasa kusikiliza utabili wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA ambapo amesema kwa kipindi cha miezi mitatu hii ya mwisho wa mwaka watu sita wamepoteza maisha kwa ajali ya kufukiwa na vifusi katika mgodi wa Kinyambwiga uliopo wilayani Bunda.

sauti ya kamanda wa polisi kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa mara Mrakibu wa polisi AGOSTINO MAGERE