Mazingira FM

NMB yatoa msaada wa vifaa vya shule Rorya vyenye thamani ya milion 84

17 February 2024, 8:59 pm

Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka ameishukuru Bank ya NMB kuwa wadau wazuri wa maendeleo hasa kwa upande wa elimu.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka ameishukuru Bank ya NMB kuwa wadau wazuri wa maendeleo hasa kwa upande wa elimu.

Dc Chikoka ameyasema hayo leo wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali  vya sekta ya elimu kwa shule tano tofauti vyenye thamani ya shilingi milioni 84.

Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka
Dc Chikoka kushoto akishikana mkono na kaimu meneja wa NMB kanda ya ziwa Hamadani Silia

Kwa upande wake kaimu Meneja wa NMB kanda ya ziwa Hamadani Silia amesema wao kama banki na wadau wa maendeleo hasa katika sekta ya elimu baada ya kupokea maombi wamechangia vifaa hivyo ili kurudisha faida kwa wananchi ambao pia ndiyo wateja wao.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na madawati, mabati, pamoja na vifaa vingine vya ujenzi kwa shule tano tofauti wilayani Rorya ambavyo thamani yake ni shilingi  milioni 84.

Kaimu Meneja wa NMB kanda ya ziwa Hamadani Silia

Diwani kata ya Nyahongo Samson Kagutu amesema NMB wamekuwa wadau wazuri wa maendeleo ambapo amesema katika shule mbili atajitolea kuwafungulia akaunti wanafunzi 10 kutoka katika kata ya Nyahongo ili ushirikiano uonekane.

Diwani kata ya nyahongo Samson Kagutu