Mazingira FM

Wanahabari watakiwa kuripoti vitendo vya ukatili dhidi ya watoto

21 October 2023, 6:47 pm

Waandishi wa habari katika Picha ya pamoja mkoani Dodoma baada ya kupata mafunzo namna ya kuripoti Habari za ukatili dhidi ya watoto wa kike.

Wito umetolewa kwa waandishi habari kuripoti taarifa dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake katika jamii.

Na Fadhil Mramba

Wito umetolewa kwa waandishi habari kuripoti taarifa dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake katika jamii.

Hayo yamesemwa na afisa maendeleo mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Bi.Anna Mhina wakati akizungumza na wanahabari kutoka redio kumi na tatu za kijamii jijini Dodoma.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo

Amesema lengo kubwa la mafunzo ni kuwajengea uwezo wanahabari waweze kuandika habari kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto,mimba za utotoni,Magonjwa ya kuambikizwa na afya ya uzazi.

Ameongeza kuwa mpango wa serikali ni kuendeleleza mpango kazi wa kutokomeza ukatili kwa mwaka huu ambao unatokana na ule wa mwaka 2021 na wa mwaka huu utaenda hadi mwaka 2028.

Mmoja ya wanasemina akielezea uzoefu wake kwenye juhudi za kutokomeza ukatili kwenye jamii.

Inakadiriwa watoto 246 milioni wanafanyiwa vitendo vya ukatili kila mwaka na watoto milioni 14 wapo mashuleni pia asilimia 50 ya wanafunzi wanauelewa mdogo juu ya ukatili na unyanyasaji wakijinsia.