Mazingira FM

Mwenyekiti UWT Bunda akabidhi viti mwendo 17 kwa wenye ulemavu

3 July 2026, 9:12 am

Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Bunda, Maryciana Sabuni

Uamuzi wa kutoa msaada huo umetokana na kupokea maombi mengi kutoka kwa watu wenye ulemavu waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za usafiri na utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.”

Na Adelinus Banenwa

Viongozi na wananchi wametakiwa kutoa kipaumbele katika kuwasaidia watu wenye ulemavu ili kuboresha maisha yao na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Bunda, Maryciana Sabuni, wakati wa hafla ya kukabidhi baiskeli maalumu za watu wenye ulemavu (viti mwendo) kwa wanufaika kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Akizungumza baada ya zoezi hilo lililofanyika leo katika Ukumbi wa Heriath mjini Bunda, Sabuni amesema uamuzi wa kutoa msaada huo umetokana na kupokea maombi mengi kutoka kwa watu wenye ulemavu waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za usafiri na utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.

Sauti ya Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Bunda, Maryciana Sabuni

Baadhi ya wanufaika wa baiskeli hizo maalumu wameeleza shukrani zao kwa msaada huo, wakisema utawarahisishia usafiri, kuongeza uhuru wa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kupunguza changamoto walizokuwa wakizikabili katika maisha yao ya kila siku.

Sauti za Baadhi ya wanufaika wa baiskeli hizo