Mazingira FM

Kicheko cha mashabiki wa Yanga Bunda ushindi dhidi ya Simba

14 August 2026, 10:39 am

Mashabiki wa Simba, wamekubali matokeo hayo huku wakitaka viongozi wa klabu hiyo kuboresha kikosi,

Na Juma Hangi

Mashabiki wa Yanga wameeleza furaha yao baada ya timu hiyo kuifunga Simba bao moja kwa sifuri katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa jana, Agosti 12, 2026, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Mashabiki hao wamepongeza uimara wa kikosi cha Yanga, wakiamini usajili wa wachezaji wapya umeongeza nguvu katika timu hiyo kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Maoni ya mashabiki wa yanga Bunda

Kwa upande wa mashabiki wa Simba, wamekubali matokeo hayo huku wakitaka viongozi wa klabu hiyo kuboresha kikosi, hasa safu ya ushambuliaji.

Maoni ya mashabiki wa simba Bunda

Bao pekee la Yanga lilifungwa dakika ya 31 na mshambuliaji Albert Kangwanda kwa kichwa, na kuifanya Yanga kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa ufunguzi wa msimu mpya.

Naye Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amewapa pole mashabiki wa timu hiyo na kuwataka kusahau matokeo hayo na kuelekeza nguvu katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.