Mazingira FM

Gharama ya mafuta bado ni mwiba kwa abiria na madereva

19 August 2026, 10:30 am

Baadhi ya madereva bodaboda wakisubiri abiria

Licha ya bei ya mafuta kushuka, bado wanakabiliwa na gharama kubwa za uendeshaji, ikiwemo matengenezo ya magari, ununuzi wa vipuri, matairi na mahitaji mengine,

Na Juma Hangi

Madereva na abiria katika Mji wa Bunda, mkoani Mara, wameendelea kulalamikia hali ngumu ya maisha inayowakabili katika sekta ya usafirishaji kutokana na gharama ya mafuta, wakiiomba serikali kuingilia kati kupunguza mzigo wa gharama unaowakabili wananchi.

Wakizungumza leo, Agosti 18, 2026, baadhi ya madereva na abiria mjini Bunda wamesema kushuka kwa bei ya mafuta hakujaleta nafuu wanayoitarajia katika gharama za usafiri na usafirishaji wa mizigo.

Madereva wamesema licha ya bei ya mafuta kushuka, bado wanakabiliwa na gharama kubwa za uendeshaji, ikiwemo matengenezo ya magari, ununuzi wa vipuri, matairi na mahitaji mengine, hali inayowafanya kushindwa kushusha kwa kiasi kikubwa nauli na gharama za usafirishaji.

Sauti ya moja ya dereva
Eneo la mtaa wa Saranga mjini Bunda

Kwa upande wao, abiria wamesema gharama za usafiri bado ni changamoto, hasa kwa wananchi wanaotegemea usafiri katika shughuli zao za kila siku.

Sauti ya moja ya abiria

Wadau hao wameiomba Serikali kupitia mamlaka husika kufanya tathmini ya gharama halisi za uendeshaji wa usafirishaji na kuhakikisha wananchi wanapata nafuu pale ambapo mazingira ya soko yanaruhusu.

Wamesema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha manufaa ya kushuka kwa bei ya mafuta yanawafikia wananchi kupitia kupungua kwa gharama za usafiri na usafirishaji.

Aidha, wameitaka Serikali kuendelea kufuatilia mwenendo wa nauli na gharama za usafirishaji ili kuhakikisha wananchi hawabebeshwi mzigo mkubwa wa gharama wakati bei za baadhi ya pembejeo za usafirishaji zikishuka.