Mazingira FM

Walioko Nyatwali wapewa saa 24 kuondoka

21 September 2026, 9:49 am

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Enock Kaminyoge

Kaminyoge amesema Zaidi ya wananchi 4,176 wakilipwa fidia ya jumla ya shilingi bilioni 53.4.

Na Joseph Makori

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Enock Kaminyoge, ametoa saa 24 kwa wananchi wanaoendelea kuishi eneo la Nyatwali kuondoka, akisema eneo hilo sasa ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kuendelea kuishi huko kunaweza kuhatarisha maisha yao.

Kaminyoge amesema eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 14,250 liliongezwa kwenye hifadhi mwaka 2022, huku zaidi ya wananchi 4,176 wakilipwa fidia ya jumla ya shilingi bilioni 53.4.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Enock Kaminyoge

Amesema asilimia 95 ya waliolipwa fidia tayari wameondoka, huku asilimia 5 wakiendelea kubaki licha ya kuondolewa kwa huduma za kijamii na kuanza kusogea kwa wanyama kama tembo, simba na fisi.

Hata hivyo, amesema Serikali inaendelea kushughulikia malalamiko ya wananchi kuhusu fidia.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Enock Kaminyoge