Mazingira FM

Kichuri kutumika kutangaza utamaduni Mara

9 October 2026, 9:49 am

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evance Mtambi

Pamoja na utamaduni wa Kichuri, Mkoa wa Mara una vivutio mbalimbali vya utalii vinavyoweza kuchangia katika kukuza uchumi na kuongeza fursa kwa wananchi.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evance Mtambi, amesema Kichuri ni utamaduni halisi wa Mkoa wa Mara unaopaswa kutambuliwa na kuendelezwa kama sehemu ya utambulisho wa mkoa huo.

Brigedia Jenerali Mtambi ameyasema hayo Oktoba 8, 2026, wakati akihutubia kikao cha wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Mara, kilichokuwa na kauli mbiu “Fursa za Kiuchumi.”

Amesema pamoja na utamaduni wa Kichuri, Mkoa wa Mara una vivutio mbalimbali vya utalii vinavyoweza kuchangia katika kukuza uchumi na kuongeza fursa kwa wananchi.

Ametaja miongoni mwa vivutio hivyo kuwa ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambayo ni moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, pamoja na tamaduni mbalimbali za makabila yanayopatikana ndani ya Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa, utajiri wa tamaduni na vivutio vya utalii vilivyopo Mara unatoa fursa kwa wadau wa maendeleo kuwekeza na kuibua shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazoweza kunufaisha wananchi.

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutambua, kutunza na kuendeleza tamaduni za jamii zinazopatikana mkoani humo, huku zikitumika pia kama sehemu ya kukuza sekta ya utalii na uchumi wa Mkoa wa Mara.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evance Mtambi