Mazingira FM

Utoro ukosefu wa uzio bado changamoto shule ya Dr Nchimbi

3 October 2026, 7:43 am

Mkuu wa Shule ya sekondari Dr Nchimbi Mwalimu Benard Ngassa akizungumza katika mahafali ya 19 ya kidato cha nne ya shule hiyo

Changamoto hizo zimetajwa katika risala ya wanafunzi wa kidato cha Nne wakati wa mahafali yao ya 19

Na Juma Hangi

Imeelezwa kuwa Shule ya Sekondari Dr. Nchimbi iliyopo wilayani Bunda, Mara, inakukabiliwa na changamoto za utoro, ukosefu wa mahitaji ya wanafunzi na nidhamu, hali iliyosababisha baadhi yao kushindwa kuendelea na masomo.

Changamoto hizo zimetajwa katika risala ya wanafunzi wa kidato cha Nne wakati wa mahafali yao ya 19, ambapo wanafunzi 261 wanatarajiwa kuhitimu, huku wakiomba upatikanaji wa chakula na kuanzishwa kwa masomo ya amali, sayansi na kompyuta.

Risala ya wanafunzi
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne Dr Nchimbi wanahotarajia kufanya mtihani wa kuhitimu hivi karibuni

Aidha, wanafunzi wameomba kuongezwa mabweni kwa Kidato cha Tano na Sita pamoja na nyumba za walimu, huku Mkuu wa Shule ya sekondari Dr Nchimbi Mwalimu Benard Ngassa akiomba kujengwa kwa uzio na ukumbi wa shule. Amesema shule ina madarasa na maabara za kutosha kwa masomo ya vitendo.

Sauti ya Mwalimu Benard Ngassa
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Dr Nchimbi

Akijibu risala hiyo, mgeni rasmi amewataka walimu na wanafunzi kuongeza juhudi ili kuboresha ufaulu na kuondokana na Daraja la Nne na Sifuri. Pia ameahidi kuleta cherehani shuleni hapo kwa ajili ya kuwajengea wanafunzi ujuzi wa vitendo na kuwawezesha kujiajiri.

Majibu ya mgeni Rasmi