Mazingira FM

Kufutwa sheria ya utaifishaji mifugo kicheko kwa wafugaji

8 September 2026, 8:19 am

Moja ya changamoto zilizokuwepo nipamoja na mifugo kukamatwa ijumaa kisha kwa weekend inakwenda kuuzwa  ikidaiwa haina mwenyewe.

Na Adelinus Banenwa

Mwenyekiti wa wafugaji taifa Mrida Mshota ameipongeza serikali kwa kufuta sheria ya utaifishaji mifugo akisema uamuzi huo unakwenda kuleta kicheko kwa wafugaji kutokana na kero kubwa waliokuwa wakiipitia.

Mrida ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha @asubuhileo kinachorushwa kupitia @mazingirafm Sept 7, 2026 ambapo amesema zaidi ya kaya milioni 25 tanzania nzima hivyo uamuzi huo wa serikali umepokelewa kwa furaha na wafugaji.

Amesema moja ya changamoto zilizokuwepo nipamoja na mifugo kukamatwa ijumaa kisha kwa weekend inakwenda kuuzwa  ikidaiwa haina mwenyewe hali iliyokuwa inawafanya wafugaji waendelee kuwa masikini

Aidha ametoa rai kwa wafugaji kuwa  mbali na kufutwa kwa sheria hiyo wanatakiwa kuzingatia mipaka na kuacha tabia ya kuingiza mifugo kwenye hifadhi na kwenye maeneo ya wakulima.

Sauti ya Mwenyekiti wa wafugaji taifa Mrida Mshota