Mazingira FM
Mazingira FM
9 September 2026, 11:21 am

Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini wahusika wa tukio hilo.
Na Adelinus Banenwa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limethibitisha kutokea kwa tukio la kuuawa kwa Daud Komanya, dereva wa pikipiki maarufu bodaboda, baada ya kushambuliwa na watu wasiofahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo, amesema Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kwa lengo la kuwabaini na kuwakamata watu waliohusika na tukio hilo.
Akizungumza na Mazingira FM, Kamanda Lutumo amesema taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini wahusika wa tukio hilo.