Mazingira FM
Mazingira FM
8 August 2026, 7:11 pm

Kwa mujibu wa sheria, wananchi wanapaswa kutumia wataalamu wa sheria katika kusimamia na kuandaa mikataba ya mauziano, ili kuhakikisha taratibu za kisheria zinafuatwa na kulinda haki za wahusika.
Na Adelinus Banenwa
Wakili Aloyce Kaditanus amesema wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na watendaji wao hawana mamlaka ya kusimamia mikataba ya mauziano, ikiwemo ya ardhi na mali nyingine hata kama ni baiskeli.
Amesema hayo leo Aug 8, 2026 wakati akitoa elimu ya masuala ya kisheria katika kipindi cha Ufahamu wa Sheria, kinachorushwa na Radio Mazingira FM.

Wakili Aloyce amesema kwa mujibu wa sheria, wananchi wanapaswa kutumia wataalamu wa sheria katika kusimamia na kuandaa mikataba ya mauziano, ili kuhakikisha taratibu za kisheria zinafuatwa na kulinda haki za wahusika.
Amesema endapo kutatokea mgogoro kuhusu mkataba, wakili aliyesimamia na kusaini nyaraka hizo anaweza kuitwa kutoa ushahidi kuhusu mchakato wa makubaliano hayo.
Amewataka wananchi kuzingatia sheria na kutumia wataalamu husika wakati wa kufanya mauziano, hatua ambayo amesema itasaidia kupunguza migogoro, hususan ya ardhi, inayojitokeza katika jamii.