Mazingira FM

Mazingira Fm yatoa mshindi tuzo za EJAT 2022

23 July 2023, 9:35 pm

Catherine Msafiri Madabuke mtangazaji radio Mazingira na mshindi wa tuzo ya Umahiri katika kipengele cha utalii na uifadhi. Picha kutoka mtandaoni

Radio Mazingira Fm imefanikiwa kumtoa mshindi wa tuzo za EJAT zinazotolewa na baraza la habari Tanzania MCT ambaye ni Catherine Msafiri Madabuke.

Na Adelinus Banenwa

Catherine Msafiri Madabuke mtangazaji kutoka radio Mazingira fm ameibuka mshindi wa umahiri wa uandishi wa habari katika kipengele cha utalii na uhifadhi tuzo za EJAT 2022.

Tuzo hizo zinazotolewa na baraza la habari Tanzania MCT kwa waandishi wa habari mahiri ambapo tuzo za mwaka 2022 zimetolewa usiku wa tarehe 22 july 2023 katika ukumbi wa mlimani city Dar es salaam.

Akitangazwa mshindi

Ikumbukwe kwamba ni kwa mara ya pili Radio mazingira fm inatoa mshindi wa umahiri wa buandishi wa habari katika tuzo hizi amabapo mwaka 2020 Thomas Masalu mtangazaji wa mazingira fm aliibuka mshindi wa tuzo hii ya umahiri wa uandishi wa habari katika kipengele cha utalii na uhifadhi

Kwa niaba ya uongozi wa radio Mazingira Fm inampongeza Catherine Msafiri Madabuke kuibuka mshindi katika tuzo hizo.