Mazingira FM

DC Naano; akemea tabia za wafanyabiashara kupandisha bei za vyakula wakati wa Ramadhani.

25 March 2023, 7:42 pm

Ikiwa waislamu nchini Tanzania na duniani kote wameanza mwezi kufunga katika mwezi  mtukufu wa Ramadhani wafanyabiashara wamelalamikiwa desturi ya kupandisha bei ya bidhaa za chakula vinavyotumika katika kipindi hiki.

Wakizungumza kupitia kipindi cha asubuhi leo kupitia radio mazingira fm leo March 23, 2023 wamesema ni jukumu la serikali kuchukua hatua kwa kusimamia ongezeko la bei kwenye vyakula katika kipindi hiki.

maoni ya wananchi

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe. Dr Vicent Naano amesema wao kama serikali wilayani Bunda anatoa wito kwa wafanyabiashara kuacha tabia ya kupandisha bei bidhaa za chakula zinazotumika katika kipindi hiki cha Ramadhani kama vile mihogo, viazi, sukari miongoni mwa bidhaa nyingine maana wataobainika hatua kali zitachukuliwa.

DR VICENT NAANO

Aidha Dr Vicent ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara wenye  tabia ya kuwaibia wanachi  katika masoko wanakata amboni (sadolin) wakati wa kuwauzia wananchi mahindi ambapo amesema jambo hilo ni uhujumu wa wazi.

DR VICENT NAANO