Mazingira FM

Mhe Maboto ataja mafanikio jimbo la Bunda mjini 2023

27 December 2023, 12:45 pm

Mhe Robert Chacha Maboto Mbunge Jimbo la Bunda Mjini

Mhe Robert Chacha Maboto Mbunge Jimbo la Bunda Mjini amesema Kwa Mwaka huu 2023 amefanikisha miradi mbalimbali kufanyika Kwa upande wa Afya, Elimu, miundombinu pamoja na Maji.

Na Adelinus Banenwa

Mhe Robert Chacha Maboto Mbunge Jimbo la Bunda Mjini amesema Kwa Mwaka huu 2023 amefanikisha miradi mbalimbali kufanyika Kwa upande wa Afya, Elimu, miundombinu pamoja na Maji.

Mhe Maboto ameyasema hayo wakati akizungumza na redio Mazingira Fm ambapo amesema mwaka huu ulipoanza vipaumbele ilikuwa hasa kwenye Maji, umeme, elimu miongoni mwa mipango mingine.

Aidha Mhe Mbunge amefafanua kuwa kwa mwaka 2023 amefanikisha jumla ya mitaa 24 kutoka Jimbo la Bunda Mjini kupata umeme wa shilingi elfu 27 badala ya 320,000. Upatikanaji wa fedha za ujenzi wa mradi wa Maji Misisi – Zanzibar, Manyamanyama – Mgaja pamoja na mradi unaoendelea wa Balili – Rubana – Kunzugu, shule mpya tatu ambazo mbili ni za msingi Shule ya msingi Azimio Nyasura na Shule ya msingi Bunda stoo pamoja na shule ya Sekondari ya Bunda Mjini.

Kuelekea sikukuu ya mwisho wa mwaka Mhe Maboto amewatakia sikukuu njema wananchi wote wa Jimbo la Bunda Mjini kusherekea Kwa Amani huku akiwataka kuendelea kuiunga mkono serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasan.