Mazingira FM

Mara waikubali ZUKU, waipokea kwa mikono miwili

22 September 2023, 2:53 pm

Rahimu Razack, Afisa mauzo ZUKU Kanda ya Mwanza. Picha na Thomas Masalu.

Wananchi wa mkoa wa Mara wameoneshwa kuridhishwa na huduma ya king’amuzi cha ZUKU kutokana na ubora wake wa muonekano wa picha.

Na Thomas Masalu

Wananchi wa mkoa wa Mara wameoneshwa kuridhishwa na huduma ya king’amuzi cha ZUKU kutokana na ubora wake wa muonekano wa picha pamoja wingi wa chanel huku gharama akiwa ni chini.

Hayo yamejiri leo kupitia kipindi cha asubuhi leo cha radio Mazingira fm wakati wa mahojiano na wawakilishi wa ZUKU mkoa wa Mara ambapo kupitia simu za wasikilizaji wameonyeshwa kurudhishwa na huduma huku wakiomba waendelee kutoa huduma Bora yenyewe uendelevu.

Akijibu maswali ya wasikilizaji Rahimu Razack ambaye ni Afisa mauzo ZUKU kanda ya Mwanza amesema ZUKU kipindi hiki wamekuja upya zaidi na wameboresha katika kitengo cha huduma ili kuendelea kuwapa huduma bora wateja.

Pamoja na hayo amewaomba wasikilizaji kuendelea kununua ving’amuzi vya ZUKU ili kuendelea kupata habari na burudani kikamilifu.