Mazingira FM

Adaiwa kuuawa na mpenzi wake, mwili watelekezwa ndani Bunda

22 August 2023, 4:11 pm

Jeshi la polisi mkoa wa Mara linaendelea kumtafuta mhusika wa tukio hilo huku akibainisha baadhi ya vitu vilivyopotea katika nyumba ya marehemu vimekamatwa wilayani Serengeti.

Na Adelinus Banenwa

Jeshi la polisi mkoani Mara linamtafuta mwanaume mmoja anayetuhumiwa kumuua mwanamke aliyetajwa kwa jina la Pelesi Sumuni anayetajwa kuwa mpenzi wake maeneo ya Nyasura D kata ya Nyasura halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara.

Akizungumza na Mazingira fm kamanda wa polisi mkoa wa Mara ACP  Salum Ramadhan Morcase amesema ni kweli tukio hilo limetokea na kama jeshi la polisi wanaendelea kumtafuta muhusika wa tukio hilo huku akibainisha baadhi ya vitu vilivyopotea katika nyumba ya marehemu vimekamatwa wilayani Serengeti.

ACP  Salum Ramadhan Morcase

Aidha amewataka wananchi kuachana na tabia za ukatili hasa kwa migogoro inayohusiana na wivu wa kimapenzi na pindi wanaposhindwa kuelewana basi waachane kwa amani.

ACP  Salum Ramadhan Morcase

Diwani wa kata ya Nyasura Mhe Magigi Samweli Kiboko amewataka wananchi na wakazia wa nyasura kuwa natabia ya kujitambulisha kwa viongozi pindi wanapoamia kwenye maeneo mapya ili waweze kutambulika na ikitokea wamepata tatizo iwe rahisi kupatiwa msaada.

Wito huo umetokana na utata wa kifo cha Pelesi Sumuni mkazi wa kata hiyo ambapo mhe kiboko aliiambia mazingira fm kuwa tukio hilo ni baya na halikubaliki kwenye jamii.

Mhe Magigi Samweli Kiboko

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyasura D Manga Makone ameiambia mazingira fm kuwa tukio hilo limetokea tarehe 16 AUG 2023 ambapo alipata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusiana na mwananchi kuonekana ndani kwake akiwa amelala katika mazingira yaliyotiliwa shaka kwa kuwa hata baada ya kuamshwa hakuamka.

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyasura D Manga Makone