Mazingira FM

Mbunge Bunda mjini akabidhi taa stendi ya mabasi Bunda

10 December 2023, 11:28 am

Katibu wa mbunge ndugu Kija mwenye shati jeupe akikabidhi taa Kwa viongozi wa kituo Cha mabasi Bunda. Picha na Adelinus Banenwa

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto ametoa taa za 3 wati 100 kwa chama cha mawakala wa mabasi stendi kuu ya mabasi Bunda

Na Adelinus Banenwa

Mbunge wa jimbo la bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto ametoa taa za 3 wati 100 kwa chama cha mawakala wa mabasi stendi kuu ya mabasi Bunda kwa lengo la kuwasadia kuepukana na giza

Katibu wa mbunge jimbo la Bunda mjini Ndugu Emmanuel Kija. Picha na Adelinus Banenwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mhe mbunge Maboto , katibu wa mbunge jimbo la Bunda mjini Ndugu Emmanuel Kija amesema taa hizo alizozitoa Mhe Maboto zimetokana na maombi ya chama hicho ambayo waliyawasilisha mbele ya mbunge kama kero alipofika katika kituo hicho cha mabasi kusikiliza kero zao.

Katibu wa CCM wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa.

Ndugu Kija ameongeza kuwa pia Mhe mbunge ametoa benchi mbili za kukalia abilia ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi yake aliyoitoa kwa chama hicho.

Kwa upande wao baadhi ya watumiaji wa stendi wakiwemo mawakala wa mabasi, wafanyabiashara na madereva pikipiki wamemshukuru Mhe Maboto kwa kuwaletea taa hizo ambapo wamesema imekuwa kero kwao kufunga biashara mapema kutokana na ukosefu wa mwanga pindi giza linapoingia angali stendi hiyo ni kubwa hapa Bunda.