Mazingira FM

Bunda TC yatakiwa kukamilisha miradi kwa wakati

15 May 2026, 10:43 am

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salum Mtelela

Madiwani pamoja na wataalamu wa halmashauri wana wajibu wa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo kuanzia hatua za mwanzo hadi kukamilika kwake.

Na Thomas Masalu

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salum Mtelela, ameielekeza Halmashauri ya Mji wa Bunda kuhakikisha inasimamia kikamilifu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya halmashauri hiyo ili ikamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

Maagizo hayo ameyatoa Mei 14 mwaka huu wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, ambapo alisisitiza kuwa usimamizi madhubuti wa miradi ni msingi wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo yaliyokusudiwa na serikali.

Mtelela amesema madiwani pamoja na wataalamu wa halmashauri wana wajibu wa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo kuanzia hatua za mwanzo hadi kukamilika kwake, ili kuhakikisha fedha zinazotolewa na serikali pamoja na mapato ya ndani zinatumika ipasavyo.

Sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salum Mtelela
makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda Daniel Marko aliyeshika kipaza sauti akiwa mkurugenzi wa halamshauri ya mji wa Bunda Juma Haji

Aidha, amesisitiza suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani, akieleza kuwa kuongeza juhudi katika ukusanyaji huo kutaiwezesha halmashauri kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi pamoja na kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salum Mtelela