Mazingira FM

WAFUNGWA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO NA BUNDUKI,

4 March 2022, 6:00 pm

Washitakiwa wanne wa Ujangili wamefungwa kila mmoja kifungo cha miaka 20 katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kwa kukutwa na meno manne ya tembo na bunduki aina Riffle 458 kinyume cha Sheria.

Waliokumbwa na adhabu hiyo katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 3/2018 mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Serengeti Adelina Mzalifu ni Khamisi Gamaho (37) mkazi wa kijiji cha Robanda,Hamisi Bwanana(34) mkazi wa kijiji cha Bwitengi,Ginena Bwanana(34)mkazi wa kijiji cha Bwitengi wilaya ya Serengeti.

Mwingine ni Karimu Mussa Mkazi wa kijiji cha Mwaseni Kibiti Mkoa wa Pwani ambaye ilibainika kuwa ndiye mtaalam wa kuua tembo kazi ambayo alijifunzia katika mapori yaliyoko mikoa ya Pwani na alikuwa anakodiwa kwa Sh300,000 kwa tukio moja.

Mapema leo Ijumaa Machi 4 Wakili wa Serikali Donasian Chuwa mbele ya Hakimu Mzalifu iliyokuwa na ulinzi mkali wa askari wenye silaha ameikumbusha mahakama kuwa wote walikuwa wanakabiliwa na makosa manne ya uhujumu uchumi.

Amesema,Januari 3,2018 katika kijiji cha Robanda wilaya ya Serengeti washitakiwa walikamatwa na nyara za Serikali ambazo ni meno manne ya tembo,kosa la pili walikamatwa na wakimiliki silaha aina ya bunduki Riffle 458 kinyume cha Sheria.

Amesema kosa la tatu ni kukutwa wakimiliki risasi 3 na kosa la mwisho ni kuua tembo wawili kinyume cha Sheria.

Amesema,kwa pamoja tarehe hiyo saa 4 asubuhi walikutwa wamelala ndani ya nyumba ya Gamaho huku meno ya tembo yakiwa yamefichwa ndani ya mchanga wa kujengea,na baada ya kubanwa walitoa silaha na kisha wakaenda kuonesha mizoga miwili ya tembo waliokuwa wamewaua ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mzalifu amesema,kila kosa kila mmoja anatumikia kifungo cha miaka 20 hivyo adhabu zote zinakwenda