Mazingira FM

Mwanri: kulima kwa mstari kutaongeza uzalishaji kwa wakulima wa Pamba

14 March 2022, 6:23 pm

Balozi was Pamba Tanzania Mh Agrey Mwanri akiwaonesha wakulima Baadhi ya mche wa Pamba ulioshambuliwa na wadudu

Balozi wa Pamba Tanzania Mh Agrey Mwanri amesema mwitikio wa wakulima wa zao la Pamba Wilayani Bunda wa kulima kwa mstari umekuwa mkubwa tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo wakulima walikuwa wanalima kwa kulusha mbegu

Hayo ameyasema Leo 14 march 2022 Huko Hunyari Halmashauri ya Wilaya ya Bunda katika siku ya pili ya ziara yake kwa wakulima wa Pamba Wilayani Bunda Balozi huyo wa Pamba nchini amesemaKiwango ilichowekewa Wilaya ya Bunda Cha uzalishaji wa Tani elfu 50 ambazo ni sawa na Asilimia 62.5 kwa Mkoa zitafikiwa endapo wakulima watazingatia upuliziaji sahihi wa dawa na muda wa kupulizia

balozi Mwanri akionesha kichwa cha pampu ambacho hakitakiwi kutumiwa na wakulima wa Pamba kwenye kunyunyizia viuadudu

Amesema pia upandaji kwa mstari ambao unazingatia sentimita 60 kwa 30 kwa ekari ambapo mkulima atakuwa na jumla ya miche 44,444 tofauti na mwanzo ambapo mkulima alikuwa akipata miche 22,222 kwa ekari moja

Kwa upande wao wakulima wamesema wameipokea elimu inayotolewa na Balozi huyo hasa ya kupanda mbegu za Pamba kwa mstari na itasaidia kuongeza uzalishaji