Mazingira FM

Mwalimu mkuu adaiwa kubaka, kulawiti na kumnywesha sumu mwanafunzi wake

13 March 2024, 6:26 pm

Vitendo vya ukatili kwa watoto hasa ubakaji na ulawiti vimeendelea kushamiri Kanda ya Ziwa licha ya serikali na mashirika mbalimbali kupinga vitendo hivyo, juhudi za maksudi zinahitajika kumaliza tatizo hili.

Na Adelinus Banenwa

Tukio hilo linatajwa kutokea Machi 9, 2024, kata ya Kisorya halmashauri ya wilaya ya Bunda wakati mtoto huyo alipoachwa nyumbani kwa mwalimu kwa lengo la kuwaangalia watoto.

Mama mzazi wa binti huyo [mhanga] ameiambia Mazingira Fm kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 8 mtoto wake alienda shule lakini hakurudi nyumbani.

”Siku ya Ijumaa mwanangu alienda shule ila hakurudi nyumbani alibaki huko kwa mwalimu mkuu kwa kuwa mke wa mwalimu mkuu ni ndugu yetu, watoto wangu wanamuita dada” alisema mama huyo.

Aidha mama huyo aliongeza kuwa siku ya tarehe 9 dada yake na mtoto [mke wa mtuhumiwa] alimuacha nyumbani ili kuwaangalia watoto kisha yeye kuelekea kanisani ambapo mtuhumiwa [mwalimu mkuu] inadaiwa alipata nafasi ya kutenda unyama huo.

Mama huyo anasema baada ya kupata taarifa ya mtoto wake kuumwa kutoka kwa kaka yake mkubwa ambaye ndiye mtu wa kwanza kumuona alimuelekeza kumpeleka kituo cha afya Kisorya.

” Siku ya tarehe 9 nilipata taarifa kutoka kwa kijana wangu mkubwa ambaye amepanga karibu kwa mwalimu akiniambia mbona mdogo wangu anasema anaumwa na amelala nimemkuta hapa nyumbani”

Mama mzazi wa binti

Inaelezwa kuwa baada ya kufika kituo cha afya Kisorya wauguzi walibaini mtoto amebakwa ndipo walipoitaka familia kuchukua fomu namba 3 kutoka polisi [PF3] ili waendelee kumhudumia ambapo baada ya kaka yake kufika polisi alitakiwa kufika na mhanga ambapo alifanya hivyo ndipo wakapewa fomu hiyo ili akapewe matibabu.

Mama huyo ameendelea kuiambia Mazingira Fm kuwa wakati wanaendelea kupata matibabu kituo cha afya Kisorya hali ya mtoto iliendelea kuwa mbaya hadi ambapo siku ya Jumapili kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Naano ilifika kituo cha afya Kisorya na baada ya kuona hali ya mtoto huyo ililazimu kupewa rufaa kwenda hospitali ya Bunda DDH kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mama mzazi wa binti

Mama huyo ameiomba serikali kuchukua hatua kwa mhanga aliyetenda unyama huo kwa mtoto wake.

Mama mzazi wa binti

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney Naano akizungumza na Radio Mazingira Fm amesema ni kweli tukio hilo lipo na baada ya kupata taarifa walichukua hatua za kupata rufaa ya matibabu ya mtoto huyo pia tayari mtuhumiwa ambaye anatajwa ni mwalimu mkuu wake anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na akibainika kwamba kweli ametenda tukio hilo hatua za kisheria zitachukuliwa.

Aidha DC Naano amewataka wazazi na walezi kuzingatia malezi ya watoto wao pia walimu kuzingatia miiko ya taaluma yao na kujua kuwa wao pia ni walezi.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney Naano

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Salum Morcase amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema tayari mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Morcase amesema tukio la mwanafunzi kubakwa na kulawitiwa limetokea katika kijiji cha Kisorya na aliyefanya hivyo ni shemeji yake ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule anayosoma mwanafunzi huyo.

Kamanda Morcase ameitaka jamii kubadilika na kuachana na vitendo vya kikatili huku akiwataka wazazi kuchukulia mtoto wa mwenzio kama mtoto wako.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Salum Morcase