Mazingira FM

Kabasa sekondari wampa kongole Samia ujenzi vyumba vya madarasa

5 October 2023, 11:56 pm

Wanafunzi wa kidato cha 4 Kabasa Sekondari wakiwa katika mahafali yao. Picha na Edward Lucas.

“Kabasa Sekondari ina madarasa 28 na yanayotumika ni 22 tu hivyo ina ziada ya madarasa 6”

Na Edward Lucas

Shule ya Sekondari Kabasa iliyopo Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara, imempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa shule hiyo, Godfrey Maige Maduhu wakati wa mahafali ya kuwaaga kidato cha 4 yaliyofanyika leo katika viwanja vya shule hiyo.

Mwl Maduhu amesema kwa upande wa madarasa shule hiyo haina upungufu kwani ina madarasa 28 na yanayotumika ni 22 tu na hivyo kuwa na ziada ya madarasa 6

Mwl Godfrey Maige Maduhu, Mkuu wa shule Kabasa Sekondari. Picha na Edward Lucas
Sauti ya Godfrey Maige Maduhu

Aidha sambamba na mafanikio hayo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, taarifa hiyo ya mkuu wa shule imebainisha baadhi ya changamoto zinazoikabiri shule hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa bwalo, maktaba, walimu na matundu 24 ya vyoo.

Shule hiyo iliyoanza mwaka 2004 kwa jitihada za wananchi, wadau wa maendeleo na serikali kuu kwasasa ina jumla ya wanafunzi 880 kati yao wavulana ni 418 na wasichana ni 464

Sauti ya Mwl Godfrey Maige Maduhu