Mazingira FM

Bunda. tani 15 za mbegu za pamba zapokelewa na katibu tawala Mterela

22 October 2022, 8:18 pm

Katibu tawala Wilaya ya Bunda Mhe Salam Halfani Mterela amepokea tani 15 za mbegu za pamba kutoka Kampuni ya Muhamed interpraisess

Mapokezi hayo yamefanyika Leo 19 Oct 2022 ofisini kwa mkuu wa Wilaya ambapo Katibu tawala amesema hadi hivi sasa wilaya ya bunda imeshapokea tani 500 za mbegu za pamba na leo amepokea tani 15 kati ya tani mia moja ambazo nzinaletwa na kapuni ya muhamed interprasses
aidha amewataka amcos kutenda haki katika zoezi lka ugawaji wa mbegu hizo kwa wakulima kwani atakayekiuka hatua kali za kisheria zitachukuliwa

Kwa upande wake mkaguzi wa zao la pamba wiliya ya Bunda kutoka ofisi ya Bodi ya Pamba Tanzania Ndugu Hemmed Kabea amesema maeneo ambayo yanakwenda kupata mbegu hizi ni yale yenye upungufu ambapo ni kata tisa za halmashauri ya mji wa bunda na na baadhi katika halmashauri ya wilaya ya bunda