Mazingira FM

Jamii yaaswa kuendelea kutunza vyanzo vya maji

27 September 2023, 12:24 pm

Mhandisi wa maji kutoka bodi ya bonde la ziwa victoria Joseph Masaka. Picha na Thomas Masalu.

Lengo la upimaji wa maji ya mto huo ni kutaka kubaini hali ya afya ya mto Tigite katika vigezo vya asili na vya kisayansi, kazi hiyo imefanyika leo 26 sept 2023

Na Thomas Masalu.

Maji ni kichocheo muhimu cha maendeleo katika sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini ikiwepo kilimo, biashara, utalii na viwanda katika kuzingatia hilo Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF) kwa kushirikiana na Wataalamu wa bodi ya Bonde la ziwa Victoria pamoja na wapimaji wa afya ya mto ngazi ya jamii wamefanya kazi ya upimaji maji kwenye mto Tigite ulipo kijiji cha Matongo Kata ya Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.

Lengo la upimaji wa maji ya mto huo ni kutaka kubaini hali ya afya ya mto Tigite katika vigezo vya asili na vya kisayansi, kazi hiyo imefanyika leo 26 sept 2023.

Wakizungumza wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo Dotto Manyeli mwenyekiti wa watumia maji Nyamongo na Mwita Seri mwenyekiti wa watumiaji maji Tigite chini wamesema wao jukumu kubwa walilonalo ni kuendelea kuwakumbusha wananchi kutunza vyanzo vya maji kwa manufaa ya kizazi kijacho huku wakishukuru Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF) kwa kazi kubwa wanayoifanya katika jamii hasa suala la uhifadhi wa mazingira.

sauti za viongozi watumia maji
Elimu ikiendelea kutolewa Kwa wanafunzi namna ya kutunza vyanzo vya maji, Picha na Thomas Masalu.

Aidha wenyeviti hao wamesema kuna kila haja ya kuwepo mpango mzuri wa ugawanaji maji ili kila kundi litumie maji hivyo bodi kabla ya kutoa kibali cha kutumia maji iwe ina jiridhisha wingi wa maji kwanza ndipo inatoa kibali ili kuondoa migogoro ya namna ya kutumia maji hayo.

sauti za viongozi watumia maji

Joseph Mligo ni makamu wa Shule ya Sekondari Matongo anasema kazi iliyofanywa na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF) kwa wanafunzi waliopo katika klabu ya mazingira shuleni hapo ni kubwa ambapo wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa mabalozi wazazzi na walezi huko nyumbani na jamii kwa ujumla kwa kuwaelimisha athari zinazotokana na kushindwa kuhifadhi mazingira.

sauti ya makamu wa shule

Kwa upande wake Joseph Masaka mhandisi wa maji kutoka bodi ya bonde la ziwa victoria anayeshughulika mazingira amebainisha umuhimu wa zoezi liliyofanyika leo.

sauti ya mhandisi wa maji

Hata hivyo Mhandisi Masaka ametoa rai kwa jamii kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili viendelee kuwa safi ukizingatia kuwa maji ni uhai na uchafuzi wa maji unapotokea athari nyingi hujitokeza katika maisha ya binadamu

sauti ya mhandisi wa maji

Uchafuzi wa maji ni matokeo ya shughuli za binadamu, kwa namna ambayo huathiri vibaya matumizi yake halali ambapo hupelekea hupunguza uwezo wa vyanzo vya maji kutoa huduma za mfumo ikolojia ambao ungetoa.

Vyanzo vya maji ni pamoja na maziwa, mito, bahari, chemichemi ya maji, hifadhi na maji ya ardhini hivyo uchafuzi wa maji hutokea wakati uchafu unapoingizwa kwenye vyanzo hivo vya maji.