Mazingira FM

Wakazi wa Balili Bunda walia na ukosefu wa maji safi na salama

22 August 2023, 3:21 pm

Wakazi wa Balili wakiwa wanachota maji katika moja ya kisima ambacho hakijafunikwa. Picha na Mussa Matutu

Changamoto ya uwepo wa huduma ya uhakika ya maji safi na salama inavyowatesa wakazi wa Balili katika kata ya Balili halmashauri ya Mji wa Bunda.

Na Mussa Matutu na Samweli Erastus

Wakazi wa mtaa Balili Stoo kata ya Balili halmashauri ya mji wa Bunda, wanakabiliwa na changamoto ya huduma ya maji safi na salama hali inayotajwa kuwa kikwazo katika maendeleo.

Hayo yamebainishwa leo na wakazi wa mtaa huo wakati wakizungumza na redio Mazingira fm, ambapo wamesema kwa wale wanaotumia kisima ni kwamba hakijafunikwa hivyo kuwa na hatari ya usafi na usalama wa maji yake.

Aidha kwa wale wanaotumia mabomba ya idara ya maji changamoto imekuwa maji kutoka usiku tu wakati watu wamelala wakati matumizia ya maji ni mchana.

kwa upande wake diwani wa kata ya Balili Thomas Tamka amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema yeye kama mwakilishi amechukua hatua mbalimbali ili kuwasaidia wananchi wa Balili.