Mazingira FM

Bunda; Mhe Silinde ataka ujenzi wa madarasa ya sekondari unaoendelea ukamilike kwa wakati Bunda

28 November 2022, 10:16 pm

 

Naibu waziri wa TAMISEMI mh. David Silinde amemtaka mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua Nassari kusimamia na  kuhakikisha ujenzi wa madarasa unaoendelea katika shule mbalimbali ndani ya wilaya unakamilika kwa wakati ili mwezi wa kwanza wanafunzi watumie madarasa hayo.

Mh. Silinde ameyasema hayo alipotembelea shule ya Bunda Sekondari katika ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa madarasa unaoendelea shuleni hapo.

Pia Mh. Silinde amewataka wale wote  wanaosimamia ujenzi wa madarasa kuhakikisha wanasimamia kwa weredi na kwamba watakao shindwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua.

Katika hatua nyinge naibu waziri Mh. David Silinde amewapongeza halmashauri ya mji wa Bunda kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuhakikisha ujenzi