Mazingira FM

WWF yatembelea mashamba ya wakulima waliopatiwa mafunzo ya kilimo bora

27 September 2023, 3:14 pm

Baadhi ya Mashamba ya wakulima waliopata mafunzo kutoka WWF, Picha na Thomas Masalu.

Shirika la WWF kwa kushirikiana na watalaamu wa bodi la bonde la ziwa Victoria wametembelea wakulima waliopatiwa mafunzo ya mbinu ya kilimo bora.

Na Thomas Masalu

Shirika la WWF kwa kushirikiana na watalaamu wa bodi la bonde la ziwa Victoria wametembelea wakulima waliopatiwa mafunzo ya mbinu ya kilimo bora kitakachosaidia utuzaji wa Mazingira na vyanzo vya maji.

Mafunzo hayo yalifanyikia chuo cha kilimo cha Mogabiri wilaya ya Tarime kwa siku 10 yaliyofadhiliwa na WWF ambapo Mafunzo yalifanyika kwa nadharia na vitendo.

Miongoni mwa wakulima ambao wametembelewa na WWF ni pamoja na Sister Maria Cecilia Kasanda wa Baraki sisters Farm wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Sister Maria Cecilia Kasanda wa Baraki sisters Farm wilaya ya Rorya Picha na Thomas Masalu.

Akizungumza na radio Mazingira akiwa shambani, Sr Maria Cecilia Kasanda amesema kuwa hadi sasa hivi ameshaanda hekari 8 kwajili ya kulima kilimo bora kinachozingati mbinu zote katika utuzaji wa Mazingira.

Sr Cecilia amesema wanatarajia kulima kilimo mseto ( Mahindi, maharage na miti) katika mashamba hayo huku wakizingatia hatua zote za kilimo bora.

Aidha Sr Cecilia amesema tayari naye amefundisha watu 9 mbinu za kilimo bora ambapo 5 kutoka Bakari sisters Farm na watu 4 kutoka nje ( jamii) katika kijiji cha Bakari wilaya ya Rorya.

Hata hivyo Sr Cecilia ameshukuru WWF wa mafunzo waliyoyatoa maana yamesaidia kuwanuia katika elimu ya kilimo bora tofauti na hapo mwazoni walivyokuwa wanalima.