Mahundi achangia tani mbili za saruji zahanati ya Tiringati
12 December 2023, 4:59 pm
Mhe Naibu waziri wa maji Maryprisca Mahundi amechangia tani mbili za saruji katika zahanati ya Kijiji Cha Tiring’ati.
Na Adelinus Banenwa
Mhe Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi amechangia tani mbili za saruji katika zahanati ya kijiji cha Tiring’ati ikiwa ni ombi la Mhe Mbunge wananchi wasaidiwe kumalizia zahanati hiyo ili waanze kupata huduma.
Mhe Mbunge jimbo la Bunda Mhe Boniphas Mwita Getere amesema zahanati hiyo imekwama kuendelea na ujenzi kutokana na bajeti ya vigae (tails) hivyo ameomba badala ya kusubili vigae iwekwe sakafu ya kawaida ili huduma ianze mara Moja Kwa kuwa tayari wataalam wapo.
Kauli hiyo ya mbunge Getere imemfanya Naibu waziri wa maji Mhe, Maryprisca Mahundi kuchangia tani hizo mbili za saruji ili kuunga mkono jitahidi za wananchi na serikali katika huduma za afya