Mazingira FM

Zaidi ya asilimia 95 ya pamba yanunuliwa Bunda

24 August 2023, 1:44 pm

Mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea, Picha na Adelinus Banenwa

Zoezi la ununuzi wa pamba linaelekea ukingoni na tayari kilo milioni saba na laki tatu  na elfu hamsini na sita zimenunuliwa kutoka kwa wakulima wilayani Bunda.

Na Adelinus Banenwa

Zaidi ya tani elfu 7 za pamba tayari zimenunuliwa katika vituo vya AMCOS wilayani Bunda huku ikitajwa asilimia 95 ya pamba tayari imenunuliwa kutoka kwa wakulima.

Hayo yamebainishwa na mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda mkoani Mara ndugu Hemed Kabea wakati akizungumza na Mazingira Fm ofisini kwake ambapo amesema zoezi la ununuzi wa pamba linaelekea ukingoni na tayari kilo milioni saba na laki tatu  na elfu hamsini na sita tayari zimenunuliwa kutoka kwa wakulima na zoezi linaendelea vizuri.

Ndugu Kabea ameongeza kuwa jukumu lililopo kwa sasa ni wakulima wa zao la pamba kung’olea maotea na kuyachoma moto kama ambavyo maelekezo ya kilimo cha zao hilo yanaelekeza.

Mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea

Katika hatua nyingine Kabea ameiambia Mazingira Fm kuwa tayari maelekezo aliyoyaacha  balozi wa pamba Tanzania mhe Aggrey  Mwanri  ya uanzishwaji wa mashamba darasa yameishaanza kufanyiwa kazi ambapo kwa halmashauri ya wilaya ya Bunda tayari mashamba darasa 385 yameanzishwa huku mashamba darasa 180 kwa halmashauri ya mji wa Bunda yakianzishwa.

Mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea