Mazingira FM

Bunda: Mtoto wa miaka 15 ashikwa Mamba wakati akinywesha mifugo mtoni

27 November 2022, 2:32 pm

Gunje malemi Gunje 15 mkazi wa Kunzugu kata ya Kunzugu Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi kunzugu ameshikwa mamba wakati akinywesha mifugo mto Rubana.

Akizungumza na Mazingira fm baba mzazi wa mtoto huyo Malemi Gunje Amesema taarifa za mtoto wake alizipata kutoka kwa wasamalia wema wa waliompigia simu majira ya saa nane mchana tarehe 26 Nov 2022 kumjulisha kwamba mtoto wake aliyekwenda machungani ameshikwa mamba


” Ilikuwa saa nane mchana nikiwa nyumbani simu iliita nilipoipoikea mtu akaniambia mtoto wako ameshikwa mamba Huku mtoni niliishiwa na nguvu nikaanza kupiga yowe nikajikokota kuelekea mtoni tulitafuta mpaka saa kumi na mbili jioni lakini hatukufanikiwa kupata chochote” Amesema Mzee Malemi.

“Leo tena tumeamka saa kumi na mbili asubuhi tumetafuta mpaka saizi saa sita hakuna chochote tumerudi nyumbani kupumzika mpaka jioni tena”

Kwa upande wake Shuhuda wa tukio hilo Nyanda Henga mkazi wa kunzugu amesema wakati anachunga alisikia yowe ya mtoto akiomba msaada na alipofika sehemu ambapo yowe ilikuwa ikitoka alimkuta mtoto akilia akidai mwenzake ameshikwa mamba wakati akinywa Maji

Henga ameongeza kuwa hakuwa na jinsi ya kuingia kwenye maji maana alikuwa mwenyewe ndipo alipoamua nayeye kupiga yowe Hadi hapo wananchi wengine walipofika na kuanza kutafuta.

“Nilikuwa mbali kidogo nikichunga gafla nikasikia yowe nikaacha mifugo yangu nikafata yowe inapotokea nilipofika nikakuta mtoto mdogo analia akidai mwenzake wakati anakunywa maji mtoni mamba amemrukia na kuzama naye majini, kwa kuwa nilikuwa peke yangu na sikuwa na simu nikakosa Cha kufanya ikabidi nipige yowe ndipo alikuja mwenzetu mmoja tukachukua simu kuwajulisha wanakijiji kuhusu kilichotokea.

Xxxxxxx

Radio Mazingira Fm bado inafanya jitihada za kuwatafuta viongozi wa Mtaa na Halmashauri kujua zaidi juu ya tukio hili na Namna wanavyo yashughulikia

Usikose Update….