Mazingira FM

RC Mtanda; Wanaotakiwa kumaliza mgogoro huu ni wananchi wenyewe

26 October 2023, 8:47 pm

Mhe Saidi Mtanda katika kikao na wananchi wa vijiji vyenye mgogoro, Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe Saidi Mohamed Mtanda amewataka wananchi wa Vijiji vya Mekomariro kutoka Wilaya ya Bunda na Remong’orori kutoka Wilaya ya Serengeti kuhakikisha wanakaa na kutafuta suluhu ya mgogoro unaoendelea.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe Saidi Mohamed Mtanda amewataka wananchi wa Vijiji vya Mekomariro kutoka Wilaya ya Bunda na Remong’orori kutoka Wilaya ya Serengeti kuhakikisha wanakaa na kutafuta suluhu ya mgogoro unaoendelea.

Mhe Mtanda amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika eneo linalozozaniwa kati ya Vijiji hivyo viwili lililodumu Kwa miaka 70 ambao unadaiwa ulianza tangu 1947.

Mhe Mtanda amesema jukumu la kupata suluhu ya kudumu ni kazi ya wananchi wenyewe Kwa kuwa wao ndiyo waathirika wakubwa wa mgogoro na kazi ya viongozi ni kuwasimamia.

Wananchi wa Mekomariro na Remong’orori Picha na Adelinus Banenwa

Aidha mkuu huyo wa mkoa ametoa onyo Kwa mwananchi yeyote atakayesababisha vurugu na kusababisha uvunjifu wa Amani kwamba serikali haitasita kuwachululia hatua Kali za kisheria.

Katika hatua nyingine Mhe Mtanda amesema iwapo hawatafikia makubaliano baina ya pande zote katika mzozo huo basi atashauri mamlaka zilichukue na kuweka Taasisi za serikali kama vile kambi za jeshi

Baadhi ya viongozi wa walioambatana na mkuu wa mkoa katika utatuzi wa mgogoro. Picha na Adelinus Banenwa.

Kwa upande wao wananchi wa Mekomariro na Remung’orori wamesema wameupokea ushauri na maelekezo ya mkuu wa mkoa na kwamba ni vema wakae chini ili kupata suluhu ya kudumu.