Mazingira FM

DC Bunda,awataka viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda kujitathmini kama wanatosha kwenye nafasi zao

2 November 2022, 8:16 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Joshua Nassari amewataka viongozi wa halmashauri ya wilaya ya bunda kujitathimini kutokana na usimamizi duni wa miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Mhe Nassar ameyasema hayo leo Nov 2 katika ziara yake wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.


Mhe. Nassar amesema haiwezekani kila jambo la maendeleo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Bunda lazima liwe na dosari akitaja kama vile zoezi la sensa, amwani za makazi, madarasa ya uviko miongoni mwa mambo mengine.

Aidha amewataka viongozi wa kata, vijiji na mitaa kutokuwa kikwazo katika kutekeleza ujenzi wa madarasa katika awamu hii kwa kuwa maelekezo ya serikali yameishatoleawa kwamba viashiria vyovyote vilivyopo karibu na maeneo ya shule jamii ishiriki kuvisogeza wakiwemo na wanafunzi.

Vilevile amezitaka kamati za ujenzi, mapokezi na manunuzi zishiriki kikamilifu katika usimamizi ili ujenzi uweze kutekelezeka vizuri.

Mhe DC NASSAR amezitembelea shule za Bunda Sekondari na Sazira kwa Halmashauri ya Mji wa Bunda ambapo ujenzi wa madarasa unaendelea katika hatua mbalimbali.

kosa

Na shule za nyamang’uta, Salama, Mikomalilo na shule ya Sekondari ya Mihingo zote zipo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo ujenzi katika shule hizo haujaanza katika hatua yoyote.