Mazingira FM

Afisa kilimo Bunda auliwa na mke wake ikidaiwa chanzo ni wivu wa mapenzi

3 April 2024, 7:02 am

Pichani kushoto ni Afisa kilimo [marehemu kwa sasa] akiwa na mke wake [mtuhumiwa].

Afisa kilimo Bunda auawa na mke wake sababu zikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Na Adelinus Banenwa

Afisa kilimo bunda auwa na mke wake sababu zikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Julius Rubambi [38] afisa kilimo kata ya Neruma halmashauri ya wilaya ya Bunda amepoteza maisha kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya mwili wake

Mwenyekiti wa Kijiji Cha kibara stoo Mtaki Didas Nyagabona ameiambia Mazingira Fm kuwa tukio hilo limetokea asubuhi ya saa mbili tarehe 2 April 2024 baada ya kutokea ugomvi kati ya wanandoa hao.

Nyagabona amesema Afisa kilimo huyo amepoteza maisha akiwa anaendelea kupatiwa matibabu hospitali ya kibara baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya kifuani, miguuni na mabegani na mke wake anayejulikana kwa jina maarufu kama mama Gift.

Mbali na kumchoma na kitu chenye kali pia kwa mujibu wa shuhuda ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema pia mtuhumiwa [mke] alimng’ata marehemu sehemu za siri pua pamoja na ulimi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kijiji Cha kibara stoo Mtaki Didas Nyagabona

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Salum Morcase amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mtuhumiwa wa tukio hilo kuwa ni Elizabeth Steven [30] ambaye kwa sasa amelazwa hospitali ya Kibara akiwa chini ya ulinzi wa polisi kutokana na yeye kujeruhiwa katika tukio hilo na uchunguzi wa tukio hilo linaendelea.

Sauti ya Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Salum Morcase
Sauti ya Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Salum Morcase – wito wake kwa jamii