Mazingira FM

DC Bunda atoa siku 14 shule ianze kupokea wanafunzi

26 April 2026, 12:37 pm

Linapotajwa jambo la dhamani ya fedha kwenye mradi si tu miundombinu imara bali hata miundombinu hiyo kutoa huduma kwa wakati ili malengo ya serikali yaweze kufikiwa.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge ametoa siku 14 kwa mkurugenzi wa halamshauri ya mji wa Bunda, afisa elimu wa halmashauri Pamoja na diwani wa kata ya Nyasura kuhakikisha shule ya msingi Victoria inaanza kupokea wanafunzi na wanaanza kusoma.

Shule hiyo iliyo kata ya Nyasura halmasjhauri ya mji wa Bunda mkoani Mara imejengwa kwa lengo la kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika shule ya msingi ya Nyasura

Baadhi ya viongozi katika zoezi la upandaji miti shule ya msingi victoria maadhimisho ya miaka 62 ya muungano

Mhe mkuu wa wilaya ametoa maagizo hayo wakati wa zoezi la upandaji miti shuleni hapo katika maadhimisho ya siku ya Muungano yaliyofanyika leo April 26 , 2026 ambapo jumla ya miti 500 imepandwa katika shule hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema linapotajwa jambo la dhamani ya fedha kwenye mradi si tu miundombinu imara bali hata miundombinu hiyo kutoa huduma kwa wakati ili malengo ya serikali yaweze kufikiwa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge