Mazingira FM

Kadi 42 za bima zatolewa kwa watoto wenye mahitaji maalumu Bunda

8 August 2025, 11:54 am

Baadhi ya watoto wakikabidhiwa kadi za bima za afya

Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuhakikisha watoto hao wanapata huduma za afya kwa urahisi na usalama.

Na Taro Michael

Jeshi la Polisi  kwa kushirikiana na waendesha baiskeli wa twende Butiama wametoa msaada wa kadi za bima ya afya kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum shule ya msingi Mazoezi.

Katika tukio hilo  jumla ya kadi 42 kati ya 80 zenye thamani ya tsh 210,000  Ikiwa na maana kifurushi ni watu sita  na Kila kifurushi ni shilingi elfu 30000 zilizolengwa zimekabidhiwa kwa wanafunzi walioainishwa kuwa na uhitaji maalum wa huduma ya afya.

Moja ya watoto wenye mahitaji Maalumu akikabidhiwa kadi za bima za afya

Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuhakikisha watoto hao wanapata huduma za afya kwa urahisi na usalama.

Pia Twende Butiama nayo imeungana katika jitihada hizo kwa kutoa viti mwendo 5 pamoja na baiskeli 5 kwa wanafunzi wenye ulemavu, ili kuwawezesha kufika shuleni kwa urahisi zaidi.

Moja ya mtoto mwenye uhitaji maalum akikabidhiwa msaada wa kiti mwendo

Vifaa hivyo vimekabidhiwa rasmi na Bi. Agriphina Mmasi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni msimamizi /kiongozi upande wa wanawake Wilaya ya Bunda.

Sauti ya Agriphina Mmasi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi

Akizungumza baada ya kupokea misaada hiyo, Mwalimu Lucy Mlaki kwa niaba ya mkuu wa shule pamoja na wazazi, ameshukuru shukrani Jeshi la Polisi na msafara wa  Twende Butiama kwa moyo wa kujitoa kusaidia watoto wenye uhitaji.

Ameeleza kuwa msaada huo ni wa thamani kubwa na umeleta matumaini mapya kwa wanafunzi na familia zao

Sauti ya Mwalimu Lucy Mlaki