Watoa taarifa za uongo zoezi la uboreshaji wapiga kura waonywa
9 September 2024, 4:39 pm
Udanganyifu wa umri kwenye zoezi la uandikisha na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni kosa kisheria.
Na Adelinus Banenwa
Zikiwa zimesalia siku mbili kutamatika kwa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa Mkoa wa Mara,Simiyu na viunga vyake Imeelezwa kuwa udanganyifu wa umri kwenye zoezi la uandikisha na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni kosa kisheria.
Akizungumza na Mazingira FM kupitia kipindi cha Asubuhi leo Afisa mwandikishaji kuoka jimbo la Bunda mjini Bi Adelina Mfikwa amesema mbali na udanganyifu wa umri pia udanganyifu wa aina yoyote itambulike ni kinyume na sheria, kama vile kujiandikisha zaidi ya mara moja miongoni mwa udanganyifu mwingine.
Aidha amewataka wakazi wa jimbo la Bunda mjini wenye sifa za kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kufika kwenye vituo kwa kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza katika zoezi hilo.
Ikumbukwe zoezi la uandikishaji na uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura kwa mkoa wa Mara, Simiyu na baadhi ya halmashauri kwa mkoa wa Manyara lilianza tangu tarehe 4 September 2024 na linatarajiwa kutamatika tarehe 10 September 2024.