

5 May 2025, 11:47 am
Maadhimisho ya siku ya urithi wa dunia ambayo yatafanyika Eneo la Mugumu wilaya Serengeti mkoani Mara na mgeni rasmi inatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara.
Na Adelinus Banenwa
Kamishna msaidizi mwandamizi Stephano Msumi ambaye ni mkuu wa hifadhi ya taifa ya Serengeti amewaomba wananchi kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya urithi wa dunia ambayo yatafanyika Eneo la Mugumu wilaya Serengeti mkoani Mara na mgeni rasmi inatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara.
Maadhimisho ya siku ya urithi wa dunia ambapo yanahusisha maeneo yaliyotambuliwa kuwa ni maeneo ya urithi ambapo kupitia kikao cha 38 cha kamati ya shirika la umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO kiliamua maadhimisho hayo kufanyika tarehe 5 May kila mwaka.
Msumi ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanayofanyika Serengeti ni chini ya kauli mbiu inayosema “majanga na migogoro ni tishio kwa urithi wa dunia
Msumi amesema miongoni mwa majanga na migogoro ambayo yanasumbua urihi wa dunia hasa kwa upande wa Serengeti ni pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi, migogoro ya mipaka kati ya hifadhi na wananchi, migogoro kati ya wanyama na wananchi
Muhifadhi Zuberi Mabie Meneja wa kituo cha Michoro ya kondoa Irangi amesema kwa Tanzania maadhimisho haya yameanza kuadhimishwa mwaka 2020 huko zanzibar 2021 kilwa 2022 Zanzibar 2023 kilimanjaro 2024 kondoa na mwaka huu 2025 maadhimisho yanafanyika Serengeti.
Zuberi ameongeza kuwa tangu waanze kuadhimisha mwitikio wa wananchi kuyatambua maeneo yaliyohifadhiwa ni mzuri ambapo wananchi pia wanapata fursa ya kushiriki kwa kuonesha vitu vya utamaduni wao.
Naye Anajoyce Thadeo Kalumuna afisa program wa kitengo cha utamaduni kutoka Tume ya taifa UNESCO amesema wao kama tume mara nyingi ni kiunganishi kati ya UNESCO makao makuu na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na taasisi mbalimbali za kijamii na kiraia katika kuhifqdhi maeneo ya urithi wa dunia.
Anajoyce ameongeza kuwa tume pia inashiriki katika utekelezaji wa mikataba mbalimbali ambayo serikali kama vile Tanzania imeingia ikiwemo mkataba wa 1972 unaohusika na utunzaji na kuhifadhi maeneo ya asili na utamaduni kama ilivyo hapa Serengeti.
Kwa mujibu wa Kamishna msaidizi mwandamizi Stephano Msumi mkuu wa hifadhi ya taifa ya Serengeti amesema kwa hapa Tanzania maeneo saba yapo kwenye urithi wa dunia amabyo ni Hifadhi ya taifa ya Serengeti, Mamlaka ya hifadhi za ngorongoro, hifadhi ya taifa ya mlima kilimanjaro , maeneo ya michoro ya miambani ya kondoa, pori la akibalaSelous, magofu ya kilwa kis