Mazingira FM

Auawa na kiboko saa tano usiku

22 April 2024, 10:04 am

Picha kutoka mtandaoni

Mwanaume wa miaka 55 Bunda auawa na kiboko saa tano usiku akiwa kandokando ya bwawa.

Na Edward Lucas

Juma Ryoba Waise maarufu Kebuchwa(55)mkazi wa Kijiji cha Mihingo amefariki dunia baada ya kushambuliwa na mnyama kiboko katika bwawa kijiji cha Mihingo Halmashauri wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Tukio limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 5 wakati mwanamume huyo alipokuwa anapita njia iliyokaribu na bwawa hilo ambalo aliingia mnyama kiboko tangu usiku wa juzi tarehe 19 April 2024 na wananchi walianza kufanya juhudi za kumuondoa bila mafanikio.

Mbusiro Mnanka, ni mwenyekiti wa kitongoji cha Werya amesema alipokea taarifa ya Kiboko kuingia katika bwawa hilo tangu jana majira ya asubuhi lakini kufikia usiku saa tano kuelekea saa siba ndipo alipopata taarifa ya mtu kuuawa kutokana na kiboko huyo.

Sauti ya Mbusiro Mnanka, mwenyekiti wa kitongoji cha Werya

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mihingo, Mwita Magige Weibina amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama wakali na mamlaka zinazohusiana na uhifadhi wa wanyama pori kuchukua hatua za haraka pindi zinapopokea taarifa ya wanyama wakali kuvamia makazi ya wananchi.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Mihingo, Mwita Magige Weibina