Mazingira FM

RITA Bunda yapata tuzo ya kitaifa kwa huduma bora

14 July 2026, 5:16 pm

Afisa Msajili Msaidizi wa RITA Wilaya ya Bunda, Josephat Laulian kushoto akikabidhi hati ya pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mhe. Aswege Enock Kaminyoge

Kwa sasa mwananchi anayekamilisha taratibu za usajili ana uhakika wa kupata cheti chake cha kuzaliwa ndani ya saa 48 tangu anapowasilisha maombi.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mhe. Aswege Enock Kaminyoge, ameipongeza Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Wilaya ya Bunda kwa kupata tuzo na kushika nafasi ya tatu kitaifa kutokana na utoaji bora wa huduma za usajili wa vizazi na vifo kwa wananchi.

Sauti ya Aswege Enock Kaminyoge

Akizungumza baada ya kupokea pongezi hizo, Afisa Msajili Msaidizi wa RITA Wilaya ya Bunda, Josephat Laulian, amesema mafanikio hayo yametokana na kujituma kwa watumishi na kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma kwa wakati.

Laulian amesema kwa sasa mwananchi anayekamilisha taratibu za usajili ana uhakika wa kupata cheti chake cha kuzaliwa ndani ya saa 48 tangu anapowasilisha maombi.

Afisa Msajili Msaidizi wa RITA Wilaya ya Bunda, Josephat Laulian kushoto akikabidhi hati ya pongezi kwa katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela

Aidha, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia huduma zinazotolewa na ofisi hiyo, akibainisha kuwa mbali na huduma za usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vifo, RITA Wilaya ya Bunda sasa imepewa mamlaka ya kutoa huduma za ufilisi na udhamini, huduma ambazo awali zilikuwa hazitolewi katika ngazi ya wilaya.

Amesema hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa huduma za kisheria kwa wananchi na kupunguza gharama pamoja na muda wa kusafiri kufuata huduma hizo nje ya wilaya.

Sauti ya Joseph Laulian