Mazingira FM
Mazingira FM
9 June 2026, 11:58 am

Njiwa Manga anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya familia yaliyopo kata ya Buturu, Mtaa wa Majengo, Wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Na Taro Michael Mujora
Msanii wa nyimbo za Asili kutoka mkoani Mara Dicksoni Juma maarufu kama Njiwa Manga amefariki juni 7,2026 katika hospitali ya Wilaya ya Butiama baada ya kusumbuliwana ugonjwa wa kujaa maji tumboni (Ascites) kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu Elias Dickson amesema ugonjwa huo ulimsumbua kwa kipindi kirefu kabla ya Umauti kumfika. Njiwa Manga anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya familia yaliyopo kata ya Buturu, Mtaa wa Majengo, Wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Kifo cha msanii huyo kimewaacha mashabiki, ndugu, jamaa na wadau wa muziki wa asili katika majonzi makubwa kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki mkoani Mara.
kaka wa marehemu amewashukuru wananchi, marafiki na wadau mbalimbali walioshiriki katika kipindi cha matibabu.
Ikumbukwe kuwa Njiwa Manga alipata umaarufu mkubwa kupitia wimbo wake maarufu wa “Sindika”, uliopendwa na mashabiki wengi ndani na nje ya Mkoa wa Mara na kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii waliotambulika katika muziki wa asili.
Wadau mbalimbali wa sanaa wameendelea kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu huku wakimkumbuka Njiwa Manga kama msanii mwenye kipaji, aliyetoa mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza muziki wa asili mkoani Mara.