Mazingira FM
Mazingira FM
24 July 2026, 10:18 pm

Mwanzoni ilikuwa changamoto katika vijiji vya kata hiyo kwenye suala la mawasiliano hali iliyokuwa inapelekea Kwenda mbali kutafuta mawasiliano
Na Adelinus Banenwa
Diwani wa kata ya Nyamoko iliyopo wilayani Serengeti mkoani Mara Mhe Emmanuel Gabriel Saina ameupongeza mtandao wa simu wa YAS kwa kuzindua mnara ambao utasaidia kutatua changamoto ya mawasiliano kwenye kata hiyo na vijiji Jirani.
Akiwa mgeni rasmi Mhe Saina ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mnara wa YAS uliopo Kijiji cha Itununu wilayani Serengeti ambapo amesema mwanzoni ilikuwa changamoto katika vijiji vya kata hiyo kwenye suala la mawasiliano hali iliyokuwa inapelekea Kwenda mbali kutafuta mawasiliano
Amesema uwepo wa huduma hiyo kwa sasa itasaidia pia vijana kujiajili mfano kufungua za kifedha kama MIXX BY YAS Pamoja na kusajili line.

Kwa upande wake meneja wa YAS Mara ya kusini Ndugu Kharid Omary Mtwange amesema baada ya kupokea maombi kutoka kwa wakazi wa maeneo hayo na wao kama mtandao walifanya utafiti leo wamezindua mnara huo ambao anaamini utawasaidia wananchi ambao wamekuwa wakipata changamoto ya mawasiliano na yas wamekuwa wakifanya hivyo kwa maeneo yote nchini ili kuahkikisha hakuna mwananchi anakosa mawasiliano.

Awali badhi ya wakazi wa kitongoji cha Itununu ameushukuru mtandao wa YAS kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu kwa kuwa wamekuwa wakipata changamoto ya mawasiliano huku wakihamasisha wananchi wengine ambao hawana line kuhakikisha wanazipata .