Mazingira FM

Esperanto Sec yafanya mahafali ya 11, ufaulu wasisitizwa

25 September 2026, 8:27 pm

Diwani wa kata ya Ketare katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Mramba Simba Nyamkinda, katika mahafali ya 11 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Esperanto.

Amewataka wazazi kushirikiana na uongozi wa shule kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula wanapokuwa shuleni, akisema lishe bora ni sehemu muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kuwa na uwezo mzuri wa kujifunza.

Na Fadhil Mramba

Diwani wa kata ya Ketare katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Mramba Simba Nyamkinda, amesema ataendelea kushirikiana na Shule ya Sekondari Esperanto iliyopo Kijiji cha Marambeka, kwa kutoa misaada mbalimbali itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Akizungumza katika mahafali ya 11 ya Kidato cha Nne ya shule hiyo, Diwani Nyamkinda amewataka wazazi kushirikiana na uongozi wa shule kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula wanapokuwa shuleni, akisema lishe bora ni sehemu muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kuwa na uwezo mzuri wa kujifunza.

Sauti ya Mramba Simba Nyamkinda

Aidha, Nyamkinda amewataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na utabiri wa mvua za El Niño, akisisitiza umuhimu wa maandalizi mapema ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.

Sauti ya Mramba Simba Nyamkinda

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Esperanto, Mwalimu Kenedy Kishiwa, amesema pamoja na juhudi za Serikali katika kuboresha shule hiyo, Diwani Mramba Simba Nyamkinda amekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha miundombinu ya shule.

Amesema miongoni mwa misaada iliyotolewa ni pamoja na ujenzi wa maktaba ya kisasa yenye vitabu na kompyuta, maabara za Kemia na Biolojia, nyumba nane za walimu, vyoo, mabweni ya wanafunzi pamoja na kisima cha maji.

sauti ya Kenedy Kishiwa

Mwalimu Kishiwa amesema uwepo wa miundombinu hiyo umechangia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kusaidia shule hiyo kupata matokeo mazuri katika mitihani.

Shule ya Sekondari Esperanto imekuwa ya nne kiwilaya kati ya shule 27 katika mitihani ya taifa, hatua ambayo uongozi wa shule umeitaja kuwa ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kutokana na juhudi za pamoja za walimu, wanafu