Mazingira FM

Mangariba watano wasakwa baada ya mabinti watano kuokolewa ukeketaji Mara

5 November 2026, 5:42 pm

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Angelina Marco

Ukeketaji ni miongoni mwa mila zinazohatarisha maisha ya watoto wa kike, kuwakatisha masomo na kuwaweka katika mazingira ya kuozwa wakiwa na umri mdogo.

Na Adelinus Banenwa

Serikali imeagiza kukamatwa kwa Mangariba watano wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya ukeketaji wilayani Serengeti mkoani Mara, kufuatia kuokolewa kwa mabinti watano wa kidato cha kwanza waliokuwa katika mpango wa kufanyiwa ukeketaji.

Mabinti hao kutoka Kata za Rung’abure, Kebanchabancha na Nyansurura wameokolewa kupitia ushirikiano wa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marco, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jeshi la Polisi na Hope for Girls and Women Tanzania.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara Mkuu wa Wilaya hiyo, Angelina Marco, amesema Serikali haitavumilia vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyolenga watoto wa kike na itaendelea kuchukua hatua dhidi ya wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Baadhi ya wanafunzi waliokuwa kwenye mkutano wa DC

Amesema ukeketaji ni miongoni mwa mila zinazohatarisha maisha ya watoto wa kike, kuwakatisha masomo na kuwaweka katika mazingira ya kuozwa wakiwa na umri mdogo.

Aidha amewataka watoto ambao watabaini mipango ya ukeketaji kwenye familia wanazoishi wakimbilie ofisini kwake ili kupata msaada hata kama hawatakuwa na nauli yakifika mauli atailipa yeye

amewashangaa pia wazee wa kimila ambao kwa kiasi kikubwa hushawishi mila hiyo kuendelea akiwataka waache mara moja watoto hao wasome kwa kuwa serikali imekeza sana kuwapatia elimu watoto ndiyo maana elimu nibure kuanzia awali mpaka kidato cha sita

Sauti ya Angelina Marco
Baadhi ya wananchi wa Serengeti walikuwa kwenye mkutano wa DC