Mazingira FM
Mazingira FM
22 August 2026, 6:51 pm

Sababu zinazoweza kumfanya mwenye mali asimjumuisha mtoto ni pamoja na mtoto kutomuhudumia mzazi wakati akihitaji msaada au kuwa na kusudio la kumuua mzazi kwa lengo la kupata mali.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya mirathi inayojitokeza baada ya mwenye mali kufariki.
Wito huo umetolewa na Wakili Alloyce Kajitanus katika kipindi cha Uelewa wa Sheria kinachorushwa na Redio Mazingira FM.
Wananchi wamehimizwa kuandika wosia ili kuweka wazi namna mali zao zitakavyogawanywa baada ya kifo na kuepusha migogoro ya kifamilia.
Amesema sababu zinazoweza kumfanya mwenye mali asimjumuisha mtoto ni pamoja na mtoto kutomuhudumia mzazi wakati akihitaji msaada au kuwa na kusudio la kumuua mzazi kwa lengo la kupata mali au kama amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa baba yake.