Mazingira FM
Mazingira FM
8 September 2026, 10:59 am

Mpango huo unalenga kuwasaidia wafugaji kutoka katika umaskini kwa kuwawezesha kupata ng’ombe na kulipa gharama kwa kutumia sehemu ya mapato yatokanayo na uzalishaji wa maziwa.
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa mpango wa “Kopa Ng’ombe, Lipa Maziwa” unaotekelezwa kwa ufadhili wa taasisi za kifedha unatarajiwa kuwasaidia wafugaji kuongeza kipato na kujikwamua kiuchumi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Ally Manonga, amesema mpango huo unalenga kuwasaidia wafugaji kutoka katika umaskini kwa kuwawezesha kupata ng’ombe na kulipa gharama kwa kutumia sehemu ya mapato yatokanayo na uzalishaji wa maziwa.
Manonga ameyasema hayo Septemba 7, 2026, wakati akizungumza katika kipindi cha Asubuhi Leo kinachorushwa na Mazingira FM, ambapo amesema utekelezaji wa mpango huo utaanza katika Mkoa wa Kagera, katika wilaya za Misenyi na Karagwe.
Amesema mpango huo ni fursa muhimu kwa wafugaji, kwani unatarajiwa kuwawezesha kuongeza uzalishaji wa maziwa, kipato na hatimaye kuboresha maisha yao.