Mazingira FM

Bodi ya pamba yawapiga msasa wanahabari Kanda ya Ziwa

21 August 2026, 10:18 am

Afisa wa Bodi ya Pamba, Penina Range

Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya pamba iwapo vitatumika vizuri na kutoa taarifa sahihi kwa wakulima na wadau wengine

Na Angel Mbalamwezi

Bodi ya Pamba Tanzania kwa kushirikiana na STV Online imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mitano kwa lengo la kuwajengea uelewa zaidi kuhusu uandishi wa habari zinazohusu zao la pamba.

Mafunzo hayo yamefanyika mjini Shinyanga na kuwahusisha waandishi kutoka Mara, Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Geita.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Pamba Kanda ya Ziwa Magharibi, Afisa wa Bodi ya Pamba, Penina Range, amewataka waandishi kuandika habari zenye ukweli, zilizofanyiwa utafiti na kutumia takwimu sahihi.

Amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya pamba iwapo vitatumika vizuri na kutoa taarifa sahihi kwa wakulima na wadau wengine

Sauti ya Penina Range
Mkurugenzi wa STV, Sitta Tuma

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa STV, Sitta Tuma, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo waandishi, hususan wanaotoka katika mikoa inayolima pamba.

Sauti ya Mkurugenzi wa STV Sitta Tuma
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Pamba nchini, Costantine Mathiasi

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Pamba nchini, Costantine Mathiasi, amesisitiza umuhimu wa waandishi kufuata kalenda ya Bodi ya Pamba ili waweze kuelewa hatua mbalimbali za zao hilo kuanzia uzalishaji hadi kufikishwa viwandani.

Naye Mwamasishaji wa maendeleo ya zao la pamba  na Afisa kilimo kutoka bodi ya pamba Tz Edward nyawile   amesema  serikai kupitia bodi ya pamba inakuja na mikakati ya  kongani na viwanda katika kuongeza uzalishaji wenye tija ikiwa  ni pamoja na usanifu wa ubora wa pamba.