Mazingira FM

Nyatwali mbioni kulipwa

19 February 2024, 11:26 am

Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela, Picha na Adelinus Banenwa

Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela amelihakikishia baraza la madiwa la mji wa Bunda kuwa taratibu za kuwalipa wakazi wa Nyatwali zipo ukingoni na muda wowote kutoka sasa wakazi hao wataanza kulipwa.

Na Adelinus Banenwa

Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela amelihakikishia baraza la madiwa la mji wa Bunda kuwa taratibu za kuwalipa wakazi wa Nyatwali zipo ukingoni na muda wowote kutoka sasa wakazi hao wataanza kulipwa.

Baadhi ya madiwani katika kikao cha baraza Bunda mjini ,Picha na Adelinus Banenwa

Kauli hiyo ameitoa katika baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Bunda katika kikao cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023 na 2024.

Mtelela amesema kuwa suala la Nyatwali serikali inalibeba kwa uzito mkubwa na inatamani lifike mwisho ili kila mwananchi apate haki yake lakini bado adhma ya serikali iko palepale ya kulitwaa eneo la kata ya Nyatwali kwa maslahi ya uuma.

diwani wa kata ya Nyamakokoto Mhe  Emmanuel Machumu Malibwa, Picha na Adelinus Banenwa

Kauli hiyo ya mtelela imekuja baada ya diwani wa kata ya Nyamakokoto Mhe  Emmanuel Machumu Malibwa kutaka kujua ni lini serikali itawalipa wakazi wa Nyatwali au kama imeshindwa ilejeshe miundombinu iliyozuiliwa ili wananchi waendelee kupata huduma ili waepukane na adha wanazozipata kwa sasa.