Mazingira FM

NIDA Bunda: Zaidi ya vitambulisho elfu 50 vyapelekwa ofisi za kata

22 October 2023, 7:22 am

Fredson Samwel, Afisa Usajili NIDA Wilaya ya Bunda. Picha na Edward Lucas

“Mbali na vitambulisho vilivyokuwepo awali, serikali imeleta tena vitambulisho vingine kwa wale waliojiandikisha hivi karibuni kwahiyo wananchi wafike ofisi za kata kuchukua vitambulisho vyao”

Na Edward Lucas

Wito umetolewa wananchi wilaya ya Bunda mkoani Mara kufika katika ofisi za kata kwa ajili ya kuchukua vitambulisho vyao vya taifa.

Wito huo umetolewa jana 21 Oct 2023 na Afisa wa Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA Wilaya ya Bunda, Fredson Samwel kupitia Kipindi cha Sema Usikike kinachorushwa na kituo cha Radio Mazingira Fm

Amesema NIDA Wilaya ya Bunda imeleta zaidi ya vitambulisho elfu 50 ambavyo vimepelekwa katika ofisi za kata mbalimbali kulingana na mgawanyiko wa halmashauri husika hivyo kwa wale ambao hawajapata vitambulisho vyao wanatakiwa kutembelea ofisi za kata kwa ajili ya kupata vitambulisho.

Sauti ya Fredson Samwel, Afisa wa NIDA Bunda akifafanua kuhusu zoezi la vitambulisho